Afia Obinim,

Simon Makonde

Simon Makonde alizaliwa Jumatatu. Baba na mama yake waliitwa Bwana na Bi Omari Makonde. Alizaliwa mjini Mogadishu mwaka wa 1991 nchini Somalia. Bwana Omari ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi. Bi Omari Makonde hupika chakula kwenye hoteli yake.

Simon Makonde alipewa jina lake Jumanne. Jina lake makonde lina maana ya kupigana kwa kutumia mikono. Baada ya majadiliano mengi kati ya wazazi wake, jina makonde lilikubaliwa kwa sababu Simon alizaliwa wakati vita vilipoanza Mogadishu. Ili wakumbuke vita vilivyowakimbiza kutoka Mogadishu hadi Kismayu, waliamua kumuita mwana wao Makonde.

Simon Makonde alioa siku ya Jumatano. Mke wake aliitwa Rhoda. Rhoda alikuwa karani katika idara ya serikali inayoshughulika na masomo. Harusi yao ya kufana ilifanyika katika Kanisa la Uinjilisti hapo mjini Mombasa.

Simon Makonde aliugua ugonjwa wa malaria uliompata siku ya Alhamisi. Aliumwa na mbu alipokuwa akitembelea dada yake kule Mombasa. Hakuwa na neti ya kujifunika ili kujikinga na mbu

Simon Makonde alikimbizwa hadi hospitali ya wilaya ya Pwani, Ijumaa iliyofuata. Wakati wa kupelekwa kwake kwa hospitali, madaktari walikuwa katika mgomo ili kushinikiza serikali iwaongezee mishahara. Kwa hali hiyo, simon Makonde hakuhudumiwa ipasavyo na ugonjwa wake ukazidi kumlemea.

Simon makonde alifariki Jumamosi. Mwili wake ukahifadhiwa katika chumba cha maiti. Ndugu, jamaa na marafiki walizidiwa na uchungu. Mwili wake ulisafirishwa hadi Mogadishu alipozaliwa.

Simon Makonde alizikwa Jumapili huko huko Mogadishu. Mungu na ailaze roho yake mahali pema peponi.

Na hiyo ndiyo hadithi ya Simon Makonde