Afia Obinim,

Amka Kumekucha

Ewe ndugu yangu wee
Amka kumekucha
Kamata jembe na panga
Twende shamba

1
Wa ujenzi wa taifa
Kwani nicho kiini hasa
Kisababishacho njaa

2
Hata wewe mwanangu
Amka kumekucha
Kwani hizi ndizo saa
Za kwenda shule

3
Hata wewe Karani
Amka kumekucha
Kwani hizi ndizo saa
Za kwenda kazi

4
Uvivu ni adui mkubwa
Wa ujenzi wa taifa
Kwani nicho kiini hasa
Kisababishacho njaa

5
Uvivu ndio adui
Wa ujenzi wa taifa
Jiepushe na uvivu
Tujenge taifa

6
Ndugu yangu kumekucha
Amka twende shamba
Jiepushe na uvivu
Tujenge taifa

7
Mwanamke kumekucha
Amka uende shule
Elimu ndio msingi
Wa maendeleo

8
Karani kumekucha
Amka uende kazi
Jiepushe na uvivu
Tujenge taifa

9
Hata wewe Karani
Amka kumekucha
Kwani hizi ndizo saa
Za kwenda kazi