fulaira@kasahorow.com,

Amigo

Tabia zako zimeshakupasae
Mke na watoto wamekimbia
Tulikukanya chunga heshima yako
Mke na watoto wako nyumbani
Ndio hazina ya maisha yako...
Amigo, Amigo

Wakati tunakupa ushauri we
Uliona sisi watu fitina
Twaingilia mambo yako ya ndani
Na kwamba tukuache kama ulivyo
Sababu wewe bingwa wa maisha...
Amigo, Amigo

Thamani ya mke ni mavazi
kula vizuri kulala vizuri
ndio siri ya kudumisha ndoa
mtaishi kwa raha amigo
watoto wako wapeleke shule
kwa manufaa yao ya baadaye
Elimu ndio zawadi muhimu
Kwa watoto wako, Amigo
Badala yake mabo yote hayo
kwa mkeo imekuwa ni ndoto
Maisha yake ya kubahatisha
Na kazi unfanya, Amigo
Amechoka mwisho kakimbia
umebaki kulaumu wenzio
Lawama zako hazina msingi, bembeleza mkeo akurudie!

Majirani na rafiki tulishakukanya sana Amigo
Heshimu mke na watoto wako
Heshimu baba na mama nyumbani
Na wakwe zako uwape heshima
Shemeji zako pia waheshimu
Tukawa sisi wabaya kwako
Shauri wetu hauna maana
Tukwache kama ulivyo Amigo
Sababu wewe ni bingwa wa maisha
Mahari umeshalipa Amigo
Mkeo huna habari naye
Na leo yamekufika mambo

Ubingwa wako na mke amekukimbia Eh!
Ubingwa wako na mke amekukimbia Eh!
Ubingwa wako na mke amekukimbia Eh!
Ubingwa wako na mke amekukimbia Eh!